Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) –ABNA– Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, amesema kuwa utekelezaji wa usimamizi mpya wa Mlango-Bahari wa Hormuz kwa kuzingatia kanuni za kisheria utakuwa na manufaa makubwa kwa mataifa yote ya eneo hilo.
Katika sehemu ya ujumbe wake, Kiongozi huyo alieleza kuwa hatua hiyo italeta mazingira ya amani, utulivu na maendeleo ya pamoja kwa watu wa kanda, huku manufaa yake ya kiuchumi yakichangia kuongeza ustawi na furaha miongoni mwa wananchi.
Aidha, alisisitiza kuwa neema na mafanikio yatokanayo na usimamizi huo yatawanufaisha watu wa eneo zima, akihitimisha kwa maneno ya Qur'ani Tukufu: "Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hata kama makafiri watachukia."

Maoni yako